Friday, 15 May 2015

Daktari asahau simu ya Mkononi kwenye tumbo la mgonjwa..


Stori ambazo zimewahi kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari na kuingia kwenye headlines mbalimbali ni zile ambazo tunasikia mara kwa mara kuwa Daktari alikua anafanya Operesheni(Upasuaji) lakini kwa bahati mbaya akasahau mkasi au akasahau baadhi ya vifaa vingine vya Matibabu.
Leo stori ambayo nashare na wewe mtu wangu ni kuhusu Daktari ambaye alisahau simu yake ya mkononi kwenye tumbo la Mama Mjamzito baada ya kufanyiwa upasuaji,ambaye alienda kujifungua na huyo daktari ndiye aliyekua akiongoza Upasuaji huo kwa huyo mama.
Hii imetokea kwenye nchi ya Jordan na inasemwa kuwa Mama huyo aligundua hali hiyo baada ya simu hiyo kuanza kuunguruma tumboni,Taarifa ya Gulf News inasema mwanamke huyo anatambulika kwa jina la Hanan Mahmood Karim ambaye ana umri wa miaka 36, alijifungua mtoto wa kiume akiwa na uzito wa Kg 4.8

No comments:

Post a Comment