Friday, 8 May 2015

Stars kucheza na Misri, Uganda

Taifa Stars
Taifa Stars ya Tanzania itacheza mechi yake ya kuwania kufuzu kwa AFCON 2017, dhidi ya Misri Juni 13 nchini Misri, kisha kucheza na Uganda Dar es Salaam Uganda Juni 21 kuwania kufuzu kwa fainali za wachezaji wa ndani CHAN.
Kuelekea katika mchezo wake na Uganda, iliyo nafasi ya 71 katika viwango vya dunia vya FIFA, Nooij amesema kuwa michuano ya Cosafa Cup itakayochezwa Afrika ya Kusini Mei 17 itaisaidia kujiandaa na mechi hiyo pamoja na ile ya mapharao wa Misri.
Uganda imealikwa nchini Rwanda katika mashindano maalumu ya kukumbuka wanamichezo waliouawa mwaka 1994 katika mauaji ya kimbali.
Kocha wa Uganda, Mserbia Milutin ‘Micho’ Sredojevic amesema mualiko wa Rwanda utaisaidia The Cranes kujiimalisha na mechi yao dhidi ya Stars, ambayo imeiweka Tanzania nafasi ya 107 katika viwango vya FIFA

No comments:

Post a Comment