Friday, 15 May 2015

AUNT, KAJALA WAMTUKANA WEMA


Waandishi wetu
MASTAA wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel na Kajala Masanja, juzikati walikutana na kutumia muda wa takriban nusu saa (dakika 30) kumsengenya aliyekuwa shosti wao, Wema Sepetu.
Mastaa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel na Kajala Masanja.
Tukio hilo lilijiri  hivi karibuni kwenye Bustani za Ndoto Polepole zilizopo Bagamoyo, ambapo mastaa kibao walihudhuria sherehe ya Baby Shower ya Aunt, iliyokuwa imesheheni vituko kibao huku gumzo likiwa ni kutokuwepo kwa Wema.
Awali paparazi wetu aliwashuhudia wawili hao wakimzungumzia Wema tena huku watu wengine wakisikia, kubwa likiwa kumshangaa kwa namna anavyotaka kila anayekuwa rafiki yake, awe adui wa maadui zake.Mjadala huo ulikuwa mkubwa, ambapo Kajala kuna wakati alimuuliza Aunt sababu ya Wema kutokuwepo eneo hilo ndipo alipompa mkasa mzima.
Aunt akimlisha Kajala keki.
Mazungumzo hayo ya Kajala na Aunt yaliwafanya hata waalikwa wengine kumteta Wema, wakidai kuwa anatakiwa kujiangalia kwani ni staa ambaye hadumu na marafiki zake na mara nyingi wakiachana, huachana kwa ubaya.Ijumaa lilijaribu kuingilia mazungumzia hayo ili kujua kisa cha wao kutumia muda mwingi kumjadili Wema lakini wote waliishia kuguna kisha kuendelea na sherehe hiyo.

No comments:

Post a Comment