Mgomo wa wanafunzi wa Chuo Kikuu Dar ilikuwa ishu kubwa jana na pia ikapewa headlines kwenye Magazeti mengi ya leo May 20 2015.. ilianza kuzungumziwa mitandaoni hii ya leo mgomo mwingine Iringa, show ya XXL @CloudsFM ikampata mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ruaha Iringa ambaye kasimulia hali iliyovyokuwa.
>>”Tunaishi katika hali ngumu tumeshindwa kuvumilia ikabidi tuchukue hatua za kufanya mgomo ili tupewe fedha zetu.. watu zaidi ya 100 wamekamatwa wengine wamepigwa.. tumepigwa mabomu ya machozi, watu wengine wapo Hospitali“>>
“Mgomo ulianza chinichini kama siku nne zilizopita wakatuzima, ikaja barua kwamba Bodi haina hela.. hatukuwa na uhakika sana na hiyo barua ilionesha mwaka 2011 tulihisi imefojiwa.. Jana tukaanza kujipanga ili leo tufanye hii reaction.”>>—Mmoja wa wanafunzi hao.
Kamanda wa Polisi Iringa nae amepatikana na kuongelea ishu hiyo>>“Wanafunzi hawa jana walikutana usiku wamegawanyika kwenye makundi mawili, kuna kundi lilikuwa linahamasisha wenzao wagome ili waishinikize Serikali iwalipe mikopo yao.”>> Kamanda Mungi.
>>Jana walikutana kujadili njia gani waitumie kupata hiyo mikopo yao, baadhi yao walikubali wasubiri wataletewa hiyo mikopo wengine wakashinikiza kuwepo kwa hiyo migomo.. Asubuhi ya leo wengine walikuwepo darasani wengine wakataka kugoma.. Tukawa tunafatilia ambao walitaka kugoma wakawafanyia fujo wale ambao hawataki kugoma.>>
>>”Wakataka kutoka nje ya geti ili wakazuie barabara isipitike, tumewazuia kabla hawajatoka.. wamekamatwa wanafunzi 89.. tumepiga mabomu kama kuna mtu amepata mshtuko ni kwa mabomu lakini hakuna aliyejeruhiwa wala kuumizwa.>>
>>“Hali ni safi hakuna tatizo lolote.. kuna wanasiasa wameacha Bunge wamekuja huku, hatutaki mambo ya kisiasa yaingizwe kwenye mji wetu huu
No comments:
Post a Comment