Friday, 8 May 2015

RAIS JAKAYA KIKWETE atakachokifanya baada ya kuachia madaraka

Katika kuonyesha juhudi hizo, alishiriki mpango wa kuhifadhi mbwamwitu wasiangamie nchini kwa kuwa anaamini wanyamapori ni rasilimali muhimu kwa Taifa.
SHARE THIS STORY
 
 
 
0
Share
Mbwamwitu ni miongoni mwa  wanyamapori waliopo kwenye mkakati wa kuokolewa kutokana na hatari ya kutoweka kwenye hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Kubainika kuteketea kwa wanyama hao kuliibua utata kuhusu kilichosababisha tatizo hilo.
Miongoni mwa matatizo hayo ni lile lililoelezwa kuwa katika kipindi cha mwaka 1966 na 1992 walitoweka mbwamwitu wengi katika hifadhi hiyo na wengine wakihamia  Hifadhi ya Ngorongoro na Maasai Mara nchini Kenya.
Hata hivyo, watafiti wa mambo ya wanyamapori wakasema kuhama huko siyo sababu kuu inayoweza kutumika kama kigezo cha kupungua kwa mbwamwitu katika Mbuga ya Serengeti.
Sababu nyingine zikaelezwa ni magonjwa kwa wanyama walao nyama kama vile simba, dumu na chui.
Sababu nyingine ikatajwa ni kuwapo kwa mabadiliko ya tabianchi na uoto wa asili na misitu kwa ujumla inapotea na matokeo yake wanyama wanashindwa kupata hifadhi pamoja na chakula.
Sababu nyingine zinazozungumziwa ni huenda kumekuwapo kwa hujuma kutoka kwa watafiti wa nje wa wanyama hao. Hii ni kutokana na maelezo kuwa ongezeko la watafiti linakwenda sanjari na kupungua kwa wanyama hao.
Hata hivyo, ripoti za karibuni zinaonyesha chanzo ni migogoro kati ya jamii ya wafugaji na wanyama hao katika maeneo ya Loliondo.
Mbwamwitu walikuwa wanaelekea kuisha katika hifadhi hii, waliokuwa eneo la Loliondo walianza kuuawa kwa sumu kutokana na migogoro na wafugaji.
Sababu za kuwaua zinaelezwa kuwa ni kutokana na wanyama hao kushambulia na kuua mifugo kama vile mbuzi na kondoo.
Hakukuwapo na jumuisho la moja kwa moja la sababu lakini Taifa likaona kuna umuhimu wa kukoa kizazi cha wanyama hao.
Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa Allan Kijazi anasema kutokana na umuhimu wa wanyama hao shirika limekuwa likijitahidi kuwakamata na kuwahifadhi eneo maalumu ili waendelea kuzaliana.

No comments:

Post a Comment