Friday, 15 May 2015

Membe, Lowassa liwalo na liwe


SHARE BOOKMARKPRINTEMAILRATING


Na Beatrice Moses

Posted  Alhamisi,Mei14  2015  saa 10:20 AM
KWA UFUPI
Wafanya uamuzi mgumu kuhusu hatima yao majimboni. Pia, wamo Pinda, Sitta na Makinda.
SHARE THIS STORY
 
 
 
0
Share
Dar es Salaam. Makada watano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao ni miongoni mwa wanaotajwa kutaka kuwania nafasi ya urais, wamefanya uamuzi mgumu wa kutangaza kutogombea tena ubunge kwenye majimbo yao.
Wabunge hao na majimbo yao kwenye mabano ni Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta (Urambo Mashariki), Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Katavi) na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa (Monduli).
Wengine ambao wanatajwa kuutaka urais na tayari wametangaza kutogombea tena ubunge ni Spika wa Bunge, Anna Makinda (Njombe Kusini), na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe (Mtama).
Wakati wabunge hao wakitangaza kuachana na kiti hicho cha uwakilishi, wengine; Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira (Bunda), Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (Bumbuli) na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (Singida Kaskazini) wamesema watarudi tena kwenye ubunge kama watashindwa urais.
Walivyotangaza kuacha ubunge
Mei 26 mwaka 2013, Sitta alikaririwa na vyombo vya habari akisema anafikiria kustaafu ubunge, na tayari ameshawaambia wapigakura wa Urambo Mashariki juu ya azima yake hiyo.
“Viongozi wenzangu msipende kung’ang’ania madaraka. Nawaombeni mjifunze kusema yatosha…staafuni kama ninavyotaka kufanya mimi,” alisema Sitta katika Kongamamo la Mawasiliano katika Nyanja za Digitali la wanafunzi wa Idara ya Uhusiano na Masoko, Chuo Kikuu cha St. Augustine (Saut), Mwanza.
Kwa upande wake, Membe alitoa kauli ya kustaafu ubunge Januari Mosi 2013 kwenye sherehe za Mwaka Mpya nyumbani kwake. Alisema, “Unajua nimekuwa mbunge wenu kwa kipindi cha tatu. Hivi leo ninawaaga rasmi kuwa sitagombea tena nafsi hii ya ubunge.”
Lowassa, amekuwa Mbunge wa Monduli kwa zaidi miaka 20 na kutokana na azma yake ya kutaka kugombea urais,, makada kadhaa wa CCM wameanza kupigana vikumbo kumrithi.
Baadhi ya makada wanaoanza safari ya kumrithi Lowassa Monduli ni aliyewahi kuwa Katibu Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha na Diwani wa Monduli Mjini, Loata Sanare na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine, ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani marehemu Edward Moringe Sokoine.
Pinda ambaye tayari ameshatangaza nia ya kugombea urais alieleza Agosti 17, 2010 kuwa hatagombea tena ubunge katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Pinda aliirudia kauli hiyo katika mkutano wa hadhara jimboni kwake akisema muda wa kuwa mbunge umetosha na sasa anatafuta kitu kingine cha kufanya.

No comments:

Post a Comment