Wednesday, 6 May 2015

Pinda aunda kamati kusimamia usafiri



Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Samuel Sitta alisema jana kwamba kutokana na kutokea kwa mivutano baina ya wadau wa usafiri nchini mara kwa mara na kusababisha usumbufu kwa wananchi, Jumamosi iliyopita, Waziri Pinda aliunda tume itakayokuwa ikishughulikia matatizo yanayojitokeza.
SHARE THIS STORY
 
 
 
0
Share
Dar es Salaam. Wakati madereva wa mabasi, malori na daladala wakiendelea na mgomo katika mikoa mbalimbali kuishinikiza Serikali kutekeleza madai yao, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ameunda kamati ya kudumu ya kusimamia usafiri wa barabarani.
Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Samuel Sitta alisema jana kwamba kutokana na kutokea kwa mivutano baina ya wadau wa usafiri nchini mara kwa mara na kusababisha usumbufu kwa wananchi, Jumamosi iliyopita, Waziri Pinda aliunda tume itakayokuwa ikishughulikia matatizo yanayojitokeza.
“Lengo la kamati hii ni kuhakikisha kwamba wakati wote bila kusubiri migomo, kuwe na majadiliano shirikishi ya wadau wote ili kuyapatia ufumbuzi matatizo ya makundi mbalimbali katika usafiri wa barabarani,” alisema Sitta.
Aliwataja wanaounda kamati hiyo kuwa ni Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi, ambaye atakuwa mwenyekiti na katibu wake atakuwa Kamishna wa Polisi, Usalama Barabarani.
Wajumbe ni katibu mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani (Usimamizi wa Polisi na usalama barabarani) na katibu mkuu, Wizara ya Kazi na Ajira (Mikataba ya ajira kati ya Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa)/Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (Tatoa) na madereva).
Wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Masuala ya sheria), naibu katibu mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, mkuu wa uratibu na Idara ya Maafa, mwenyekiti Taboa, mwenyekiti wa Tatoa
Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Mabasi na Magari ya Mizigo, mwenyekiti wa chombo cha kusimamia haki za wasafiri na mkurugenzi wa Sumatra.
Kamati hiyo imetangazwa siku ambayo huduma za usafiri wa barabara zilisimama kutokana na mgomo wa madereva.
Mbagala mshikemshike
Mabomu ya machozi yaliyotupwa na polisi yalikuwa salama wananchi wenye magari binafsi baada ya kuwatimua mamia ya vijana waliokuwa wamefunga Barabara ya Kilwa eneo la Zakhiem na kusababisha msongamano mkubwa wa magari.
Vijana hao walifunga barabara na kuanza kushusha abiria kwenye magari binafsi na kuwalazimisha wenye magari hayo kuwapakia wanafunzi na kuwapeleka shule.
Shughuli hiyo hilo lililodumu kwa dakika 40 kuanzia saa 1.45 hadi saa 2.25 asubuhi. Vijana nao waliwashusha wafanyakazi wote waliokuwa kwenye basi la Kampuni ya Tanzania Road Haulage (TRH) waliokuwa wakienda kazini na kumlazimisha dereva kuwapakia wanafunzi na kuwapeleka shule.

No comments:

Post a Comment